Ijumaa , 17th Sep , 2021

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Mawasiliano kwa klabu ya Azam, Zacharia Thabit amethibitisha kuwa winga wake nyota, Ayoub Lyana aliyekuwa anasumbuliwa na majeraha kwasasa yupo fiti ilhali nyota mpya, Charles Zulu anataraji kukosekana kwasababu nyaraka zake za vibali hazijakamilika.

Mshambuliaji wa klabu ya Azam, Ayoub Lyanga.

Zacharia Thabiti amesema; "Ayoub alipata majeraha kwenye mechi hiyo, lakini sasa yuko fiti kuivaa Horseed. Ila mchezaji ambaye aliikosa mechi hiyo Charles Zulu ataendelea kuikosa kutokana na matatizo la nyaraka pamoja na yeye pia kuwa majeruhi".

Mbali na taarifa za wachezaji hao, Zaka amesema wanafahamu umuhimu na ugumu wa mchezo huo lakini kwa kuwa lengo la klabu hiyo ni kupata matokeo mazuri na kusonga mbele kwenye hatua ya kwanza ya mtoano kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika basi hawana budi ya kulinda ushindi wao.

"Tuko mbele kwa  mabao mawili. Tutakachokifanya kwenye mechi hiyo ni kuulinda zaidi  ushindi wetu kwasababu hata wao wanahitaji mabao 2-0 ili wasonge mbele. Tunalijua hilo na tutapambama".

Azam inataraji kucheza mchezo wake wa marudiano dhidi ya Horseed ya Somalia saa 4:00 jioni  Jumanmosi ya Septemba 18, 2021 kwenye dimba la Chamazi na mchezo huo utahesabika Horseed kuwa kwenye uwanja wa nyumbani baada ya kuchagua uwanja huo kufuatia machafuko nchini kwao.