Jumamosi , 25th Mar , 2017

Kiungo wa klabu ya soka ya Tottenham ya nchini Uingereza, Dele Alli amefungiwa michezo mitatu ya kwenye mashindano ya vilabu Barani Ulaya, kufuatia kupewa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidiya Gent mwezi uliopita.

Dele Alli akioneshwa kadi nyekundu katika moja ya mechi za UEFA dhidi ya Gent

Shirikisho la soka Barani Ulaya, UEFA limetangaza adhabu hiyo, hiyo, inayokumbusha kitendo cha Alli kumfanyia madhambi kiungo wa Gent Brecht Dejaegere, na kupewa kadi nyekundu kwenye mchezo wa Europa League, uliopigwa uwanja wa Wembley.

Adhabu hiyo, itahusisha mchezo wowote wa michuano ya vilabu Barani Ulaya, ikimaanisha Alli atakosa mechi tatu za michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu ujao, endapo Spurs, watafuzu kwenye michuano hiyo, kwa mara nyingine.

Wakati huo, huo, Arsenal nayo imepigwa faini ya pauni elfu 4,300 sawa kiasi cha milioni 12 za kitanzania baada ya mashabiki, wake kuvamia uwanja kufuataia kipigo cha 5-1 kutoka kwa Bayern Munich kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Baada ya Arsenal kupigwa 5-1 na Bayern