Ijumaa , 30th Oct , 2020

Mustakabali wa mlinzi David Alaba katika Klabu ya Bayern Munich upo mashakani kufuaia kocha Hansi Flick kusema kwamba mazungumzo ya muda mrefu ya kandarasi hayajawa na mafanikio.

David Alaba (Kushoto) akiwa na kocha wake Hans Flick baada ya kutwaa ubingwa wa 8 wa Bundesilga.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Austria mwenye umri wa miaka 28 amekuwepo Bayern tangu enzi za ujana wake mnamo 2008 na amekuwa mlinzi muhimu kwa miaka mingi.

Mkataba wa sasa wa beki huyo unamalizika mnamo 2021 Lakini mazungumzo kadhaa juu ya kurefusha mkataba kati ya mchezaji na kilabu hadi sasa yameshindwa kufikia makubaliano.

Kwakuwa Alaba atakuwa mchezaji huru katika majira ya kiangazi, Bayern inaweza kuamua kumuuza katika dirisha la uhamisho wa msimu wa baridi ili wapate kiasi cha pesa iwapo makubaliano ya pande zote mbili yatashindikana.