Jumanne , 8th Mar , 2022

Kikundi cha kuchangia figo Kidney Donor Athletes (KDA) kinachoundwa na wanachama 22 wenye figo moja kila mmoja, wanatarajia kupanda Mlima Kilimanjaro siku ya figo Duniani March 10 mwaka huu.

Kikundi cha Kidney Donor Athletes (KDA)

Lengo la kupanda mlima huo mrefu barani Afrika ni kuhamasisha watu kuchangia figo na kuionyesha Dunia unaweza ukawa na afya bora baada ya kutoa figo.

“Wote 22 tutafika katika kilele cha Kilimanjaro na kutumia miili yetu kuonyesha watu tuweza kufanya vitu vikubwa zaidi ya kukimbia nusu marathon baada ya kufanyiwa upasuaji.'' - Tracey Hulick, muanzilishi wa KDA.