Jumatano , 18th Mei , 2022

Kupitia MamaMia ya East Africa Radio Rajabu Zomboko amewashauri wanaume kuoa wanawake wanaowapenda kwa sura na maumbile na wasichunguze sana kuhusu tabia.

Picha ya Rajabu Zomboko

"Oa kwa kuangalia sura, maumbile kuhusu kuchunguza usichunguze sana, chunguza kidogo tu kwa sababu unaweza mkachunguzana kwenye uchumba na mahusiano kwa miaka lakini ndoa yenu isidumu" ameeleza Zomboko

Kipindi cha MamaMia ni kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 4:00 Asubuhi mpaka 6:00 Mchana.