Jumanne , 1st Mar , 2022

Mshauri wa mahusiano Aunt Sadaka, amesema kwamba nafasi ya mwanaume katika familia haina utofauti na ile nafasi aliyokuwa nayo mwanaume kipindi cha nyuma, isipokuwa utofauti unakuja kwenye utekelezaji wa majukumu yao.

Mshauri wa mahusiano, Aunt Sadaka

Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi Mosi, 2022, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio.

"Changamoto inakuja pale ambapo mwanaume na majukumu yake haya-reflect kwenye familia, wako wanaume wanaosimama kwenye majukumu yao vizuri sana lazima tuwapongeze, na kuna wanaume mimi ninawaita wale wa ajabu ajabu,"amesema Aunt Sadaka.