Ijumaa , 1st Apr , 2022

Siku ya Jumatatu wiki hii nchini India, alizaliwa mtoto mwenye vichwa viwili, mikono mitatu na mioyo miwili katika mwili wake.

Madaktari wanasema hawajapanga kufanya upasuaji kwa watoto hao ila wapo chini ya uangalizi.

Hii sio mara ya kwanza kwa tukio kama hili kutokea linalofahamika kama "dicephalic parapagus'' ambapo mapacha huzaliwa wakiwa wameungana.

Shaheen Khan na mumewe Sohail walitegemea kupata watoto mapacha baada ya kufanya vipimo vya ''ultrasound''na hata madaktari hawakutegemea watazaliwa wameungana, watoto hao mpaka sasa bado wapo hospitali chini ya uangalizi.