Jumanne , 26th Oct , 2021

Bilionea Jeff Bezos na mmiliki wa kampuni ya Blue Origin inayosimamia utalii wa angani ikishirikiana na kituo cha angani cha Sierra na Boeing imetangaza mpango wa kuzindua kituo cha biashara cha angani.

Picha ya Orbital Reef

Kituo hicho 'Orbital Reef' kitakuwa na ukubwa wa futi 32,000 ambapo kitawawezesha wateja kuandaa filamu katika eneo hilo, kufanya utafiti na kutakuwa na hoteli ya angani.

Katika mkutano na wanahabari kuzindua mpango huo, maafisa wakuu wa Blue Originna kituo cha angani cha Sierra walikataa kutoa gharama ya ujenzi wa kituo hicho , ijapokuwa inadaiwa wanahakika kupata ufadhili wa kitita kikubwa kutoka kwa bwana Bezos, ambaye amejitolea kutumia $1bn (£726m) kwa mwaka katika kampuni ya Blue Origin.

Tangazo hilo linajiri huku Nasa ikitafuta mapendekezo ya kuunda kituo mbadala ili kuchukua mahala pake majengo ya kituo hicho yalio angani kwa miaka 20.