Jumatano , 10th Jun , 2020

Jumanne ya Juni 9, 2020, ilikuwa ni siku maalum kwa wakazi wa Marekani hasa wale weusi baada ya kumuaga na kuzikwa kwa raia George Floyd ambaye ameuawa mikononi mwa Polisi Derek Chauvin mwishoni mwa mwezi Mei.

Watu wakibeba jeneza kuelekea kumzika George Floyd

Shughuli hiyo ya mazishi yake imefanyika Jijini Houston, Texas nchini Marekani, na kuongozwa na Kanisa la Fountain of Praise, ambapo watu takribani 500 wamehudhuria wakiwemo watu maarufu na wanasiasa wa nchi hiyo.

Gavana wa Minnesota Tim Walz, alitoa dakika 8 na sekunde 46 za ukimya ikiwa ni ishara ya heshima za mwisho za kumuaga George Floyd, aidha Mjomba wa George ametaka haki itendeke huku akisema tukio hilo ni la chuki kwa mpwa wake na wala sio uhalifu.

Polisi aliyefanya tukio hilo Derek Chauvin na wenzake wanne, wamefukuzwa kazi na wote wameshtakiwa kwa kesi ya mauaji japo siku ya jana zilitoka taarifa kwamba amewekewa dhamana ya Tsh Bilioni 2.