Jumamosi , 21st Mei , 2022

Kampeni ya Namthamini kwa mwaka 2022 inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 27 Mei, 2022 ikiwa ni muendeleo wake kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kike kusoma bila kikwazo katika shule mbalimbali Tanzania kwa kuwapatia taulo za kike.

Kampeni ya Namthamini kuzinduliwa 27, Mei, 2022

Tukio la uzinduzi rasmi wa kampeni hii litafanyika katika shule ya sekondari ya Kidete wilayani Kigamboni, Dar es Salaam, mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Fatma Nyangasa.

Huu ni mwaka wa sita kampeni hii inafanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017, ambapo kwa mwaka 2022 East Africa TV na East Africa Radio inashirikiana na Rotary Club of Dar es Salaam, Oysterbay, AMREF Tanzania na CRDB Bank.

East Africa Tv na East Africa Radio imekuwa ikiratibu kampeni hii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, ambapo kwa mwaka 2021 ilifanikisha kugawa taulo za kike za kuwaweka shuleni watoto 1500 katika mikoa mbalimbali.