Jumanne , 15th Mar , 2022

Bingwa mara 7 wa mbio za magari ya Formula 1, Lewis Hamilton ametangaza kubadilisha jina la ukoo wake kwa kuongeza jina la mama yake mzazi katika majina yake kwa sababu haelewi kwanini mwanamke hupoteza jina lake akiolewa.

Lewis Hamilton aliishi na mama yake Carmen Larbalestier mpaka alipofikisha miaka 12 na kuchukuliwa na baba yake

Lewis Hamilton amefanya hivyo kwa heshima ya mama yake mzazi Carmen Larbalestier ambaye alitengana na baba yake Anthony Hamilton tangu akiwa na umri wa miaka miwili. Alilewa na mama yake mpaka alipofikisha miaka 12 alipohamia kwa baba yake ambaye alikuwa ameoa mwanamke mwingine na kupata watoto wawili.

Lewis anataka kuttambulika kwa jina la Lewis Carl Davidson Larbalestier Hamilton.

''Kwa sababu sielewi kabisa wazo zima la kwanini, watu wanapooana, mwanamke hupoteza jina lake. Nataka jina lake liendelee na jina la Hamilton." amesema Lewis Hamilton.