Alhamisi , 10th Mar , 2022

David Bennett aliyekuwa binadamu wa kwanza Duniani kupandikizwa moyo wa nguruwe amefariki baada ya kuishi kwa miezi miwili akiwa na moyo wa nguruwe.

David Bennett akiwa hospitali.

David (57) aliyekuwa na maradhi ya moyo, alifanyiwa upasuaji Januari 7 mwaka huu nchini Marekani katika hospitali ya University of Maryland Medical Center.

Baada ya kupandikizwa moyo wa nguruwe alijumuika na familia yake baada ya wiki kadhaa na kutazama fainali za Super Bowl pamoja, na hali yake ilianza kubadilika siku kadhaa zilizopita mpaka umauti ulimpofika March 8 mwaka huu.