Jumamosi , 5th Mar , 2022

Mwanamziki Zi Faamelu ambaye mwanzo alikuwa mwanaume kabla ya kubadilisha maumbile na kuwa mwanamke, amezuiliwa kuondoka nchini Ukraine kwa sababu bado anatumbulika kama mwanaume katika vyeti vyake, hivyo anatakiwa kubaki Ukraine na kupigania taifa lake.

Zi Faamelu

Serikali ya Ukraine iliamuru wanaume wote kuanzia umri wa miaka 18 hawataruhusiwa kuondoka nchini humo kwa ajili ya kupambana katika vita ya Urusi.

Zi Faamelu ame-post video insta story akiwa analia na kuomba makundi ya haki za binadamu yamsaidie kutoka Ukraine.