Jumatatu , 14th Mar , 2022

Unaambiwa Bi Kampire Josepha (28) amekuwa akiishi bila nyusi na style ya para kichwani baada ya kunyolewa nywele na baba yake akiwa na miaka mitano ambazo hazimuota mpaka leo.

Picha ya Kampire Josepha

Kwa sasa imepita miaka 23 Kampire Josepha kuishi bila nywele hizo na kupitia mahojiano aliyofanya nchini Rwanda, anasema familia yake inaamini kubaki na upara na kutoota nywele inasabishwa na imani za kishirikana.

Aidha bibi yake amesema mjukuu wake alizaliwa na nywele ila baada ya kunyolewa hazijamuota tena, pia wamehangaika kwa mganga wa kijiji aliyewapa dawa za mitishamba kupaka ili ziote lakini imeshindikana.