Jumamosi , 25th Mar , 2017

Mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva  Mr T Touchez amesema msanii Young Dee amejiunga na lebo yake ya Touch Sound na tayari wana project zaidi ya sita.

Young Dee

 

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Mr T Touchez amesema Young Dee yupo kwenye lebo yake ya Touch Sound na kwa sasa ana meneja wake ambaye anamsimamia na pia tayari wameshatengeneza nyimbo zake zaidi ya sita lakini pia muda wowote kuanzia sasa ngoma mpya ya Young Dee itakuwa hewani.

Hata hivyo Mr.T Touchez amemalizia kwa kusema "Mimi nimeingia mkataba mrefu wa miaka mitatu na Young Dee na ataendelea kuwepo chini ya Touch Sound na mimi ndiye nitakayesimamia na kutengeneza biti za nyimbo zake zote na nia yangu ni kumfanya afanye vitu tofauti na alivyokuwa akifanya hapo awali kwa kuwa mimi namuona ni msanii mwenye biashara" 

Mr T Touchez