Ijumaa , 18th Aug , 2017

Uamuzi wa kupokea au kutopokea kielelezo cha ushahidi cha msokoto mmoja wa bangi na vipisi viwili vya bangi katika kesi inayomkabili mlimbwende wa Tanzania 2006 na muigizaji Wema Sepetu utatolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwisho wa mwezi huu

Hakimu Mkazi Mkuu mahakama ya Kisutu, Thomas Simba amewaambia mawakili upande wa utetezi na serikali kuwa uamuzi huo ulipaswa autoe leo, lakini bado kuna tafiti ambazo anazifanya na hazijakamilika hivyo wanapswa kurejea tena mahakamani  Agosti 31,2017.

Hata hivyo, baada ya kutolewa kwa uamuzi huo shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka ataendelea kutoa ushahidi wake katika kesi hiyo. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Septemba 12 na 13, 2017

Wema Sepetu wenzake wawili wanakabiliwa na shtaka la kukutwa na dawa za kulevya huku tayari vipimo kutoka ofisi ya Mkemia wa Serikali vikionyesha kwamba mkojo uliopimwa unaonyesha kuwa na vimelea vya bangi