Jumatatu , 13th Feb , 2017

Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu leo amefunguka na kuwashukuru mashabiki wake kwa kumpa faraja na kumuombea katika kipindi chote ambacho alikuwa matatizoni

Msanii wa filamu nchini Wena Sepetu akiwa na mama yake mzazi.

 

"Mimi na familia yangu tunapenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zetu za dhati kwa wote mlioshirikiana nasi kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu tulichopitia. Najua wengi mlikua mnaniombea, nashukuru kwa sala na dua zenu kwani zimenisaidia kwa kunipa nguvu wakati nikiwa kwenye wakati mgumu sana kwenye maisha yangu". Aliandika Wema Sepetu 

Wema aliendelea kutoa shukrani zake kwa wasanii pomoja na mwanasheria wake ambao walikuwa naye katika kipindi hicho kigumu katika maisha yake.
 
"Napenda kuwashukuru mashabiki wangu wote duniani kwa kuniamini na kusimama na mimi kwa kipindi chote hiki, pia napenda kuwashukuru wasanii wenzangu wote. Asante sana kwa mwanasheria wangu Alberto Msando kwa kunisimamia na kuwa na mimi bega kwa bega wakati huu mgumu. Nakuombea kwa Mungu akupe moyo huohuo wa kuwatetea wanyonge". Aliandika Wema Sepetu