Jumanne , 12th Jul , 2022

Msanii wa lebo ya Wanene Studios Mapanch Bmb ameshauri kutengenezwa kwa Maktaba ya Kihistoria ya wasanii waliotengeneza njia na kufungua milango ili wasanii wapya wajifunze.

Picha ya Mapanch Bmb kulia na kushoto ni Mansu-li

"Najivunia kuwa karibu na wasanii waliotengeneza hichi kitu tunachofanya na njia tunazopita, sio vizuri kumuona Juma Nature Fid Q unawapita. Ningeshauri wangetenezewa maktaba ya historia ili wasanii wapya wajifunze mziki kupitia wao".

Mapanch Bmb amesema hivyo baada ya kushirikishwa kwenye kazi mpya ya Mansu-li inayoitwa siku yetu.