Alhamisi , 17th Aug , 2017

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nikki wa Pili, amesema sababu ya kuiponda tasnia ya filamu ya bongo kuwa hawafanyi vizuri, ni kwamba wasanii wa tasnia hiyo wanaangalia zaidi kuuza majina yao bila kubeba maudhui ya filamu.

Nikki wa Pili

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, Nikki wa Pili amesema msanii kuwa na jina kubwa ni kitu cha muhimu kwenye filamu, lakini bila kujiwekea misingi maalum itakayokuwezesha kufanya vizuri na kufikisha filamu zako mbali, ni sawa na hakuna unachokifanya zaidi ya kuuza majina yasiyo na maana.

Msikilize hapa chini...