"Wananiita mtoto wa Magufuli" - Sholo Mwamba

Jumamosi , 27th Mar , 2021

Msanii wa muziki wa Singeli Sholo Mwamba amesema sasa hivi akitembea mtaani watu wanamwita jina la mtoto wa Magufuli na hilo limekuja baada ya kumfanya aliyekuwa Rais huyo acheze wimbo wake kipindi cha Kampeni mwaka 2020.

Kushoto ni Hayati Dkt John Pombe Magufuli, kulia ni msanii Sholo Mwamba

"Baada ya taarifa kutoka nilipokea simu nyingi sana kwamba baba yangu amefariki, kwa sababu ninavyotembea watu wananiita mtoto wa Magufuli ilikuwa ngumu kuamini kama kweli amefariki" amesema Sholo Mwamba.

Sholo mwamba ameongeza kusema Hayati Dkt John Pombe Magufuli alimuachia zawadi ya kitambulisho ambacho anaweza kuingia nacho popote kama msanii kwenye mikutano au ghafla kubwa za viongozi nchini.

Aidha kubwa zaidi atakalolikumbuka kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli  ni fedha alizozipata wakati wa Kampeni za kuwania kiti cha Urais, Ubunge na Udiwani ambapo fedha hizo zilimfanya kununua gari lake la kwanza kwenye maisha yake.

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.