Jumatano , 10th Mar , 2021

Video vixen maarufu Bongo Cappiccuno Tunda amempongeza mpenzi wake Whozu kwa kumfanya kufikisha miaka miwili kwenye maisha yake ya kimahusiano kwa mara ya kwanza kwani walishindwa wababe na matajiri.

Msanii Whozu na mpenzi wake Cappuccino Tunda

Tunda ametoa sifa hizo kwa Whozu ikiwa anasheherekea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake ambapo kupitia mtandao wa Snapchat na Instagram ameandika kuwa 

"Miaka mitatu iliyopita, mahusiano yangu ya kwanza kufikisha miaka zaidi ya miwili na bado tupo pamoja kweli nimekua

"Miaka mitatu ya kukujua sijawahi kujutia,  kukuchoka wala kutamani kuwa mbali na wewe, hongera kwa hilo mchaga sio jambo rahisi walishindwa watu wababe hadi matajiri, Happy Birthday handsome boy wangu" ameongeza 

Aidha kwa sasa kuna taarifa ambazo zinasemekana kwamba Cappuccino Tunda ni mjamzito baada ya miaka mitatu ya mahusiano yao.