Jumatano , 21st Jun , 2017

Msanii chipukizi wa bongo fleva Bright amemchana Baraka the Prince kwa kudai hana kigezo cha kumuandikia mashairi ya nyimbo zake kama jinsi anavyojinadi yeye mwenyewe

Msanii Baraka kushoto, Kulia ni Bright.

Bright amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz baada ya tetesi zilizokuwa zinavuma kuwa msanii Baraka ndiyo aliyekuwa anamwandikia mistari ya wimbo msanii huyo pindi walipokuwa chini ya uongozi mmoja.

"Baraka hana vigezo vya kuniandikia mimi nyimbo, kwanza sina madhaifu kiasi hicho, tokea naanza muziki wasanii wote niliyowashirikisha nyimbo zangu nimeandika mwenyewe. Sasa tukiongelea Baraka kuniandikia mimi wimbo au sitoweza kuja kufanya vizuri hapo utakuwa unanikosea sana, kutokana unavyojua Baraka nyimbo zake ni 'copyright' yaani kuna mtunzi, aliyefanya mix na aliyegonga biti" alisema Bright

Pamoja na hayo Bright amedai ana uwezo wa kumbadilisha msanii mwenzake aina ya uimbaji aliyokuwa nao sasa na kumpeleka mahali pengine ambapo atafanya vizuri zaidi.