Jumapili , 28th Mei , 2017

Mwanamuziki wa miondoko ya 'RnB' bongo, Ben Pol mwenye 'hit song' ya 'Tatu' amefunguka kwa kusema hawezi kujutia hata kidogo kwa kupiga picha zilizokuwa zinazomuonesha akiwa nusu uchi kwa madai alichokifanya ni kuwasilisha maudhui ya wimbo wake mpya.

Msanii Ben Pol

Ben amebainisha hayo kupitia kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV kila siku ya Ijumaa kuanzia saa tatu kamili usiku mpaka saa tano za usiku.

      Hizi ndiyo picha zilizozua gumzo mitandaoni siku chache zilizopita kama huku pata bahati ya kuziona

“Hamna majuto kwa sababu nisingeweza kutoa ‘materials’ yak u-promote wimbo wangu ambazo maudhui yake yapo tofauti na wimbo wangu…Wimbo wangu ‘message’ yake na ile sanaa yake vitu vya ku-promote lazima viwe na picha ile kwa hiyo siwezi kujikataa nikasema ngoja niiweke kidogo niisoftishe lazima niweke ule ukali, ukakasi kwa sababu ‘message’ yake na kile nilichotaka kukifikisha uzito wake lazima vifanane” alisema Ben Pol.

Bofya  hapa chini kumtazama Ben Pol alivyofunguka.