Jumapili , 28th Mei , 2017

Msanii Nyandu Tozi kutoka B.O.B Micharazo amefunguka kwa kuwaponda kundi la Weusi kuwa hawana mafanikio yoyote waliyoyapata katika maisha sababu bado wanaishi katika nyumba za kupanga.

Msanii Nyandu Tozi kutoka B.O.B Micharazo

Nyandu ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuulizwa swali juu ya ukimya wao katika muziki pamoja na mafanikio waliyoweza kuyapata kama kundi ukilinganisha na Weusi kutoka jiji la Arusha.
“Ukiniambia Weusi wana maendeleo kuliko B.O.B unanishangaza wakati wao wamepanga, B.O.B kila mtu anaishi katika ‘empire’ zao…B.O.B Micharazo ni ukoo kwa hivyo unavyoona B.O.B wapo kimya katika muziki utakuta labda sasa hivi wapo ‘busy’ mambo mengine kwa sababu watu wana majukumu yao binafsi siyo kwamba tutegemee muziki tu ‘a hundred percent no’ lazima ujishughulishe na uwe na biashara au uwe na maduka ni vitu ambavyo 'movement' vijana wengi wasa wameamka hakuna kijana ambaye amekaa tu ategemee atoe nyimbo i-hit afanye 'show” Nyandu alifunguka.
Pamoja na hayo, Nyandu amesema kundi lao la B.O.B Micharazo haliwezi kufa kutokana na ukimya wao wa muda mrefu katika ‘game’.
Katika hatua nyingine, G Nako amejibu tuhuma hizo kwa kusema “Mafanikio siyo namna vile wewe unaweza ukayatafsiri, mafanikio yangu mimi ni ku-motivate msanii wa  nje leo nimetoa ‘sound’ ya muziki mpya, mafanikio siyo pesa ‘bro’, mafanikio siyo majumba ya kifahari”
Bofya chini hapa kumtazama Nyandu Tozi alivyofunguka.