Jumatano , 29th Mar , 2017

Msanii wa hip hop Bongo Baghdad amekuwa na mawazo ya tofauti na wasanii wenzake baada ya kufunguka kwenye Planet Bongo ya EA Radio kuwa hafanyi kazi ya sanaa kwa ajili ya kipato bali anarudisha fadhila kwa watu.

Baghdad

Baghdad amesema muziki haujawahi kumpatia pesa lakini umempatia njia nyingi ya kufanya kazi ambazo zimekuwa zikimuingizia kipato na kusababisha maisha yake yasonge mbele.

"Muziki mimi naufanya kwa kurudisha fadhila, haujawahi kunipa hata 'Single cent', lakini kuna watu waliniamini wakanipatia nafasi ya kuonekana kwenye huu muziki ndiyo maana nafanya kwa ajili ya kuwaburudisha. Muziki umenipatia nafasi za kuonekana na ndiyo maana nasema narudisha fadhila" - Baghdad.

Aidha Baghdad ameongeza kuwa mchango wake umesaidia kuwafikisha asilimia 40 ya wasanii wanaosikika katika game ya bongo fleva hapo walipo na anafurahi kuona wanafanya vizuri.

"Siwafichi mimi kwa mara ya kwanza Edu Boy alinitambulisha kwa Young Killer nikatia mkono wangu, lakini Msanii wa WCB Rayvan nilimsaidia na hata mpaka anaenda Tip Top connection ulikuwa ni mpango niliouandaa, nashukuru Mungu sasa hivi yeye anaendesha gari mimi bado nadandia bajaji najivunia sana kuwa nyuma yake" - Baghdad alikazia.

Hata hivyo msanii huyo amewataka mashabiki zake wavumilie muziki anaoufanya kwa sababu amedhamiria kufanya muziki unaoishi kwa madai kwamba  mitindo huru 'free style' inasikilizwa na vijana wachache huku wazee wakiwa ndiyo wengi.