Jumatano , 28th Jun , 2017

Msanii wa bongo fleva mwenye hit song ya 'Yaongoze' Linex Sunday Mjeda amefunguka kwa kudai kwamba hamkumbuki Lulu Diva kama mwanamuziki bali anamkumbuka kama shabiki tu.

Lulu Diva kushoto na kulia ni Linex

Linex amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya ku 'blockiwa' na msanii mwenzake Lulu Diva kwa kile kinachodaiwa kuwa Linex kumtukana mwanadada huyo kwenye 'comment' ya picha aliyokuwa ameweka katika mtandao wake wa instagram.

"Inawezekana nikawa nimem-comment kama shabiki kutokana pale nilikuwa nime-post tangazo la biashara na ndiyo maana nikasema 'Kaka zako wanapokuwa mipangoni  kwamba wewe unatakiwa utulie...Wewe unaweza kukasirika kublokiwa na mtu ambaye hata haumjui ?, kwanza sidhani hata kama namba yangu anayo, sijui hata kama nimem-follow. Siyo lazima kila mtu akujue mimi mwenyewe naweza nikapita mtaa na mtu asinijue" alisema Linex.

Mtazame hapa anavyofunguka zaidi.