Jumatatu , 18th Oct , 2021

Mjasiriamali kutoka nchini Kenya, Vera Sidika pamoja na mpenzi wake Brown Mauzo wanatarajia kumkaribisha Duniani mtoto wao mwezi Novemba 1 mwaka huu.

Picha ya pamoja Vera Sidika na mpenzi wake Brown Mauzo

Queen Vee ametoa taarifa hiyo kupitia Insta story akiwajibu wakosoaji wake kuhusu ujio wa mtoto huo ambaye amekuwa akisubiriwa kwa zaidi ya miezi nane ili kuona matunda ya tumbo lake.