Jumamosi , 22nd Apr , 2017

Msanii wa muziki wa bongo fleva mwenye 'hit song ya Moyo sukuma damu' Lameck Ditto amesema yupo tayari kwa wimbo wake kufanyiwa marudio 'Cover' na msanii yoyote lakini siyo kwa lengo la kufanyabiashara.

Msanii wa bongo fleva Lameck Ditto

Ditto amefunguka hayo baada kuona watu wengi wameupokea vizuri wimbo huo na kuchezwa sehemu mbalimbali huku wasanii wanaochipukia kuonekana na wapotayari kufanya 'cover' kwa lengo la kuzidi kufikisha ujumbe mbali zaidi.

“Watu wengi wanatamani kufanya cover ya huu wimbo mimi naruhusu kiroho safi tu ila sasa wabongo wasifanye kwa kuwauzia watu unajua mtu anapofanya 'cover' kwanza kaonyesha kuikubali kazi hiyo…lakini sasa inapotokea mtu anataka kuuza hapo ndipo anaharibu kazi…akifanya cover mimi namtazama kama msanii mwenye kipaji cha ziada”. Alisema Ditto 

Kwa upande mwingine Ditto amewashukuru wananchi kwa kumpokea vizuri baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kabla ya kuja na ngoma yake ya 'Moyo sukuma damu'.