Ijumaa , 17th Feb , 2017

Msanii wa bongo fleva Shaa amesema hajawahi kujiita malikia wa uswazi bali jina hilo alipewa na mashabiki hivyo hataki kuling'ang'ania kwa kuwa halimuingizii faida yeyote.

Shaa

 

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Shaa amesema mambo ya kushindanishwa na wasanii wezake kama Vanesa na LadyJay Dee lakini yeye hajataka kuendeleza mashindano na bifu hizo kwa kuwa wasanii wa kike wapo wachache na kwamba kinachotajwa kuwa ni bifu ni mambo ya kuandaliwa na watu ikiwemo vyombo vya habari.

Hata hivyo Shaa alisema "Sina bifu na Snura na ninamkubali sana Snura ni mwanamke mpole na mnyenyekevu tulishakutana kwenye show  tukapanga tukutane siku moja na tufanya kazi ya pamoja" alisema hivyo Shaa huku akisisitiza kwamba hana bifu na msanii yeyote wakike Bongo.

Mtazame hapa kwenye show ya eNewz..............