Alhamisi , 23rd Mar , 2017

Msanii wa muda mrefu katika bongo fleva ambaye hivi sasa ameibuka na kitu kipya alichomshirikisha Peter Msechu, 'Nasema na wewe' ameweka wazi kuwa hajawahi kuandika/kuimba wimbo wenye maudhui ya mapenzi na wala hatakuja kufanya hivyo

Tabla

Akizungumza na EATV, Tabla ambaye jina lake halisi ni Elvis Geofrey Tabula amesema ameamua kujikita kwenye nyimbo zenye ujumbe wenye mafunzo kwa jamii na mara nyingi huwa anakaa kimya lakini kila anapotoka na kitu kipya mashabiki wa muziki wana muelewa.

Pia amewataka wadau wa muziki kuangalia na kutoa sapoti kwa wasanii wanaotoa kazi nzuri badala ya wale wenye kazi mbovu lakini wanatumikia 'kiki' kuteka soko la muziki.

"Mara nyingi nakaa kimya sana, ila nikileta wanaelewa. Mimi ni msanii ninayeandika vitu vinavyoishi au vinavyoigusa jamii. Sijawahi kuimba mapenzi na hata kuandika mashairi ya hivyo...... Wadau waangalie kitu kizuri si kwa sababu ni mtu flani.. waachane na wasanii ambao kabla ya kutoa nyimbo lazima watengeneze kitu kama 'kiki' vitu vinavyoshusha uhalisia wa mwanamziki na tasnia nzima pia" Amesema Tabla

Akizungumzia game ya sasa jinsi ilivyo, Tabla amesema kuwa kwa sasa sanaa ipo juu na muziki wa Tanzania umefika mbali  kiasi cha wkuingizwa katika vinyang'anyiro vya tuzo kubwa

"Game ya sasa ipo juu sana, muziki wetu umefika mbali sana kwa sasa ukiachana na Afrika, ndiyo maana leo wasanii wa hapa wanarudi na tuzo kubwa duniani".

aka Tabla. 
Song:  

Hii ndiyo kazi aliyotoka nayo Tabla kwa sasa, ikienda kwa jina la