Jumapili , 23rd Apr , 2017

Mesen Selekta ajibu kashfa ya kutaka kumpiga changa la macho Man fongo Mil 10 kwa kudai msanii huyo alishindwa kutimiza makubaliano ya kazi iliyoandaliwa na kampuni ya mawasiliano kwa kuhofia kushiriki katika wimbo mmoja na msanii Sholo Mwamba.

Sholo Mwamba na Man Fongo

"Hivi unawezaje kupewa milioni 10 ukampatia msanii laki mbili, huo ni ujinga na ninsingeweza kufanya hivyo. Mimi Man fongo sikuwa na makubaliano naye na lile halikuwa tangazo kama anavyodai. Mimi nilipata kazi kutoka kampuni ya simu ambayo ilidhamini show moja ya kuzunguka nchi nzima hivyo walitaka wasanii wafanye kitu kuhusiana na show hiyo lakini wakawa wamependekeza wasanii wanaowataka ndipo nilipokutana na uongozi wa Man fongo kujadili kazi.
Baada ya kuanza kusumbuliwa na ile kampuni mbona kazi haitoki Fongo akawa anazingua mara ukipiga simu hapokei ikipokelewa anapokea mke wake lakini tulikuja kugundua kuwa anaogopa kufanya kazi na  Sholo Mwamba" amesema Mesen Selekta.

Hata hivyo Mesen amesema baada ya migogoro iliyotokea kati ya Man fongo na Defatality music bado anamuhesabu msanii huyo kama chata wa singeli kwa kuwa ameweza kuwa msanii wa kwanza wa singeli kufanya shoo nje ya nchi.