Shindano la Dance100% lifike mikoani - Jokate

Wednesday , 28th Sep , 2016

Mrembo Jokate Mwegelo ameshauri shindano la Dance 100% lijalo lifike mikoani ili kuweza kupata vipaji vingi zaidi kuliko ilivyo sasa ambapo vijana wanaopenda kushiriki hulazimika kuja Jijini Dar es salaam.

Jokate Mwegelo

Jokate ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam aliposhiriki kutazama fainali za Dance100% zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Don Bosco Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya watizamaji.

“Ni mara yangu ya kwanza kushuhudia shindano hili nilikuwa sujui kama huwa linapendeza na kuvutia namna hii, kumbe kuna vipaji vingi sana vipo mtaani kama hapa hali niliyoiona ndiyo hii” Amesema Jokate.

Jokate ameongeza kuwa kama shindano la Dance100% litafika mikoani litaifanya jamii kuwa na muamko zaidi na kuwafanya vijana kujumuika pamoja na kufahamiana kupitia shindano hilo.

Shindano la Dance100% kwa mwaka huu limemalizika na matukio yote yataoneshwa siku ya Jumapili saa moja jioni kupitia EATV.

Aidha mwaka huu kundi la Team Makorokocho liliibuka na ushindi na kujinyakulia kitita cha milioni saba jambo ambalo limeongeza hamasa ya mashindano hayo kwa vijana wengine nchini.

Tags: 

Recent Posts

Mashabiki wa Simba na Yanga Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

Sport
Simba na Yanga watambiana matawini

Ray C akiwa studio za EA Radio

Entertainment
Ray C akumbana na 'majanga' mengine

Dkt Kigwangalla katika ziara yake, Mwananyamala

Current Affairs
Mikoa yote yatakiwa kuwa na huduma ya methadone

Ben Pol

Entertainment
Ben Pol ataja anaotamani kuwatoa