Ijumaa , 2nd Jul , 2021

Mwanamuziki Saraphina Michael ameeleza baadhi ya washiriki wa Bongo Star Search BSS wanashindwa kuendelea mara baada ya ushindi kwani wanafikiri wakishashinda ndio basi.

Mwanamuziki wa Bongofleva Saraphina Michael

Akizungumza katika Kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio, mwanamuziki huyo anayetamba na wimbo wake wa “Singo” alioimba na Baddest 47 amesema kwa sasa ameamua kuwekeza kwenye muziki kwani unahitaji nguvu kubwa.

“Wengi wakienda kushindana BSS wanafikiri akishashinda ndo basi, ila uhalisia ni kwamba baada ya kushinda kazi inaanza tena inabidi upambane kama uko underground na inasaidia kukupa platform kama mimi,” amesema Saraphina.

Akieleza elimu yake na aliwazaje kufanya vitu wili Saraphina amesema; “Kuchanganya muziki na shule haikuwa ngumu, nilikuwa na uwezo waku-balance hivi vitu viwili lakini kuna muda ilibidi ni postponed semester ya mwisho na baadae nilirudi,” amesema Saraphina.