Jumatano , 6th Jul , 2022

Ni ujumbe wa The African Princess Nandy kwa mpenzi wake Billnass kuelekea siku muhimu ya ndoa yao ambayo inasemekana itafanyika mwezi huu saba.

Picha ya Billnass na Nandy

"Nikiangalia kumbukumbu zetu nalia tu, Aaaaaaarg bwana me nimekubali tunapendana huu mwezi safari yetu inahitimishwa na Mungu, na ikawe kheri nakupenda mwenzio" ameandika Nandy

Ikumbukwe msanii wa filamu Steve Nyerere ndio ametajwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya ndoa yao.