Ray C amtamani Ray Vanny

Friday , 17th Feb , 2017

Msanii wa muziki wa bongo fleva Ray C amefunguka na kusema anamtamani sana msanii kutoka katika label ya WCB Wasafi Ray Vanny na amekuwa akipenda sana kazi zake na kuzisikiliza, hivyo anatamani kufanya naye kazi hata moja tu. 

Ray C alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema anasikia Ray Vanny anaandikia wasanii wengi sana nyimbo hivyo na yeye anatamani kufanya naye kazi kutokana na uwezo wake wa hali ya juu. 

"Nampenda sana yule mtoto Ray Vanny, anaadika sana mashairi, nasikia anaandikia wasanii wengi nyimbo hata mimi natamani kufanya naye kazi" alisema Ray C 

Mbali na hilo Ray C alimzungumzia Diamond Platnumz kama msanii ambaye amefanya mapinduzi sana na kuupeleka muziki wetu wa bongo fleva mbali zaidi 

"Kiukweli mimi nam respect sana Diamond Platnumz amefanya jambo kubwa katika muziki wetu, kama hutaki kuelewa basi tu hutaki kuelewa, japo sisi tulikuwa tunasikika sijui Kenya wapi lakini dogo amepita sehemu zingine ambazo sisi hatukufika, ambaye haelewi mchango wa Diamond katika muziki huu sijui hata ana maana gani" alihoji Ray C  

Recent Posts

Wachezaji wa Simba wakishangilia kombe lao

Sport
Simba warejea rasmi kimataifa

Donald Trump, Rais wa Marekani

Current Affairs
Marekani kujaribu kombora la masafa marefu

Kocha wa Mbao FC, Ettiene Ndayiragije Raia wa Burundi

Sport
Kocha agoma kuiacha Mbao FC

Muongozaji wa video, Nisher

Entertainment
Weusi ni ubunifu wangu - Nisher

Mlinda Mlango wa Azam FC, Aishi Salum Manula

Sport
Manula atoa kauli kuhusu kusaini Simba