Jumamosi , 25th Mar , 2017

Mkongwe wa hip hop bongo, Joseph Haule ' Prof Jay' amekanusha kuwa 'disi' wasanii wenzake akiwepo Alikiba pamoja na Afande Sele kwenye wimbo wake mpya wa 'Kibabe'.

Prof Jay (kulia) akiwa na Afande Sele

Katika ngoma hiyo, kuna mstari usemao 'Mwambieni mfalme wenu siti yangu aifute vumbi', mstari ambao umekuwa ukizusha hisia kuwa ni dongo kwa Afande Sele ambaye amewahi kupata taji ya Mflame wa Rymes. na kudai mashairi ya kawaida ambayo alimua kuyaweka. 

Akiongea kwenye eNewz ya EATV Prof. Jay amesema mstari huo ni wa kawaida na siyo dongo kwa mtu yeyote na wala hajawahi kuwa na tatizo na wasanii hao wawili hivyo ni vigumu sana kuwasema kwa kutumia wimbo kwa kuwa ni watu anaowaheshimu.

Kuhusu harakati za kisiasa, Jay amesema licha ya Afande Sele kuwa chama tofauti, si miongoni mwa wasanii waliojitokeza kumpinga wakati akigombea ubunge katika jimbo la Mikumi.

'Afande Sele mimi ninamuheshimu toka yupo CHADEMA kabla hajaenda ACT na hata wakati tunaanza harakati za kugombea kila mmoja alimtakia mwenzake kila la kheri, kingine mimi mpaka leo mtu nayemuheshimu katika utunzi wa mashairi nikiwataja kina Jay Moe basi Afande siwezi kumuacha, Alikiba mimi ni mdogo wangu na mimi ni shabiki wake analijua hilo sasa sielewi haya maneno yametoka wapi." - Alisema Prof Jay.

Huyu hapa Prof katika eNewz.....