Jumanne , 10th Jan , 2017

Producer Tiddy Hotter ambaye ametengeneza wimbo wa 'Phone' wa Ben Pol amefunguka na kusema mara nyingi amekuwa akiwapa wasanii mbalimbali 'beat' pamoja na idea za nyimbo lakini wasanii hao wamekuwa wakipotezea beat pamoja na idea hizo.

Mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva, Tiddy Hotter.

 

Tiddy Hotter amesema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo na kusema beat ya wimbo wa Ben Pol alimpa msanii wa Sappy ambaye aliomba sana japo afanye naye kazi moja na kusema alimpa beat hiyo pamoja na idea ya 'Phone' lakini baada ya hapo hakuifanyia kazi au aliipotezea hivyo akaamua idea na beat hiyo kumpa Ben Pol.

"Mimi namjua sana Sappy anapenda sana kiki, msanii wa Sappy aliniomba sana nifanye naye japo wimbo mmoja hivyo nikajaribu kumpa idea ya 'Phone' nikafanya beat nikampa nilivyoona haifanyi nikaamua kumpa Ben Pol.

Hotter aliendelea kufunguka na kujibu tuhuma za Sappy kuhusu aliyedai kuwa Ben Pol aliiba idea yake ya ngoma hiyo

"Unajuaga wasanii unaweza kumpa idea au beat harafu yeye akaipotezea na mpaka sasa nina idea nyingi nimewapa wasanii na wasipozifanya mimi nitawapa wasanii ambao wanaweza kufanya jambo na kulisimamia. Hivyo kwenye hilo suala Sappy hausiki kabisaa maana mimi sikumpa yeye bali alikuwa msanii wake bora hata huyo msanii wake ndiye angeongea maana mimi nilitaka kumpa idea hiyo msanii wake tu na si huyo Sappy" alisema Tiddy Hotter