Jumatatu , 16th Jan , 2017

Msanii wa  band ya FM Academia Nyoshi El Sadaat amesema wanategemea kuachia nyimbo mbili ambazo zimepewa majina 'Nakuita' na 'mama wa Kambo' ambazo ndizo zitakuwa kwa ajili ya mwaka huu 2017.

Nyoshi El Sadat

 

Akionge kupitia eNEWZ Nyoshi amesema kama media zitatoa sapoti ya kutosha kwa  nyimbo hizo na kukosa kufanya vizuri basi mashabiki zake wamkate mikono  na miguu ili kuweza kuficha aibu ya uso wake kwa kuwa wamejipanga vizuri na wanahakikisha wanarudisha muziki wa dansi kuwa kwenye chart.

Hata hivyo Nyoshi amesema nyimbo walizoachia kwa mwaka 2016 hazikufanya vizuri kwa kuwa hawakupata sapoti ya kutosha kutoka katika media mbalimbali hali  iliyopelekea muziki wa dansi kushuka chart kwa mwaka 2016.