"Nisamehe huko ulipo" - Msanii TID 

Ijumaa , 26th Mar , 2021

Ikiwa leo ni siku ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, msanii wa BongoFleva TID amemuomba msamaha Hayati Magufuli kwa kushindwa kufika kwenye msiba wake Wilayani Chato Mkoani Geita.

Kulia ni aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Magufuli, kushoto ni msanii TID

Akiomba msamaha huo kupitia post yake ya mtandao wa Instagram TID ameandika kuwa "Hakika Ijumaa ya leo itabaki kuwa kwenye kichwa changu, maneno peke yake hayatoshi, naomba Allah akusamehe madhambi yako, pia huko ulipo nisamehe kwa kushindwa kufika mazikoni Chato

Wasanii wengine waliondika kuhusu siku hii ya mazishi ya Hayati Magufuli ni Dogo Janja na Mwana Fa ambapo post zao zinaeleza kuwa 

"Leo ni siku ngumu sana kwa Taifa letu la Tanzania, wananchi wako tulikupenda sana lakini Mungu amekupenda zaidi, Allah akupe kauli thabiti pumzika kwa amani baba" Dogo Janja 

"Kifo hakikwepeki, na mwanadamu akitekeleza wajibu wake kwake na kwa watu wake anafikwa na kifo, naamini Mzee wangu John ‘Walwa’ Joseph Magufuli ametekeleza wajibu wake duniani ipasavyo na anakwenda akiwa amemaliza kazi iliyomleta, anakwenda akiwa na amani moyoni mwake" Mbunge wa Jimbo la Muheza, Tanga na msanii Mwana Fa