Jumapili , 16th Jul , 2017

Mbunge wa Mikumi na rapa mkongwe nchini Tanzania, Mh. Joseph Haule maarufu kama Prof. Jay amefunguka kwa kudai harusi yake imekuwa yenye baraka kutoka kwa Mungu maana ameweza kuwakutanisha viongozi wa kisiasa kwa pamoja bila ya kujali itikadi zao.

Mbunge wa Mikumi na rapa mkongwe nchini Tanzania, Mh. Joseph Haule.

Haule amebainisha hayo kupitia kipindi cha 'Friday Night Live' kinachorushwa na EATV baada ya kuulizwa ni jambo ni gani hasa liliweza kumvutia katika harusi yake.

"Kikubwa kabisa ninachomshukuru Mungu mbele za haki kabisa ni kwamba nimejitahidi kuunganisha hata siasa zetu za Tanzania ambazo zipo kwa kuwaunganisha viongozi wetu, watu wa vyama vyote walikuwa pale, watu wa dini zote walikuwa pale, kile ni kitu kikubwa kiukweli", amesema Haule.

Pamoja na hayo, Haule amedai siku mbili kabla ya harusi yake, alikuwa ni mtu mwenye wasiwasi katika nafsi yake kwamba isije ikatokea akamkana mkewe mbele ya Padri wakati wa kufungishwa ndoa.

"Nilikuwa na hofu kubwa na presha ilikuwa inapanda na ndiyo maana hata wanangu wengine sijaongea nao kwa muda mrefu hata simu yenyewe nilikuwa ninaiyogopa. Nikawa nasema isije siku Padri ananiuliza pale nikasema simtaki kabisa huyu mtu au yeye akasema hapana, kuna vitu vingi tumeshaona huko vikitokea kwa watu waliyopita kwa hiyo kusikia kile kitu kimeenda vizuri ni kitu cha kumshukuru sana Mungu ila hofu ilikuwa kubwa sana", amesisitiza Haule.

                               Maharusi wakipewa mkono wa dua mara wakati wakikamilisha Ibada ya Ndoa.

Katika hatua nyingine, Haule amesema mwanaye Lisa ameamuahidi anaenda kufaulu mtihani wake wa kuhitimu darasa la saba kwa kuwa jambo ambalo alilokuwa analisubiri kuliona kwa muda mrefu limetimia kwa wazazi wake.

Mtazame hapa anavyofunguka zaidi.