Alhamisi , 17th Aug , 2017

Rapa Wakazi amefunguka na kudai yeye ni mmoja wa wasanii ambao wamepiga show nyingi zaidi nchini Marekani kuliko hata Alikiba na wengine waliyopo Tanzania.

Wakazi amebainisha hayo baada siku kadhaa kupita msanii Malaika kujisifia kuwa yeye ndiyo msanii pekee kutoka bongo aliyeweza kufanya matamasha mengi sana nchini Marekani.

"Malaika hawezi kunifikia kufanya 'shows' kwa kule kwa sababu mwaka 2009 mimi ndiyo nilianza kutoa 'free style' za kwanza kwanza, mwaka 2010 nikatoa 'mixtape' nikawa maarufu Tanzania 'so' hizo show anazosema Malaika mimi nikawa booked kila mwaka nikawa sikai Tanzania", alisema Wakazi.

Pamoja na hayo, Wakazi ameendelea kwa kusema "ikabidi niache kazi niwe nafanya show tu hivyo hawezi kunifikia mimi. Even though nadhani hata Diamond, Alikiba sidhani kama hata hao amewafikia 'maybe' ikiwa amewapita hao saizi lakini sidhani kwa kuwa hata hao wamefanya show nyingi sasa hivi".

Kwa upande mwingine, Wakazi amedai alifikia kipindi maisha yake yote yalikuwa yanaendeshwa kwa show na wala siyo kazi nyingine kama watu wanavyofikilia.