Alhamisi , 17th Aug , 2017

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Issabela Mpanda ambaye alikuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu na msanii mwenzake Luteni Kalama, amedai kuwa kitendo cha msanii huyo kumuacha na kuoa mwanamke mwengine, alihisi amejiabisha sana.

Issabela Mpanda

Akizungumza na mwandishi wetu Issabela amesema kitendo cha kukaa kwenye mahusiano na Luteni kwa muda mrefu na kisha kumuoa rafiki yake wa karibu ambaye walikutana muda mfupi tu kilimuumiza na kumfanya ahisi kama amefanyiwa udhalilishaji mkubwa kwake.

Kufuatia kitendo hico Bella amesema anashangazwa na wasanii wenzake kutojifunza kupitia yeye, kwani karibia jamii yote ilijua kilichomsibu kwenye maisha yake.

"Nimejifunza kupitia yeye kwa sababu nilijiachia sana mitandaoni nam-posti, mwisho wa siku akaja kumuoa rafiki yangu ambaye wamekutana ndani ya wiki moja, lakini mimi na yeye tulikuwa wapenzi miaka mingi, kwa hiyo nikaona nimejiabisha kwa jamii pamoja na mashabiki zangu", alisema Issabela au Bella Fasta.

Msikilize hapa chini...