Jumatatu , 11th Sep , 2017

Msanii Nikki wa Pili amedai kuwa watanzania wengi hawajapata elimu kutokana na kuwa mfumo wa elimu Tanzania unabagua watu na ndiyo maana hata wasanii wengi hawajaenda shule na siyo kwamba hawapendi shule.

Msanii Nikki wa Pili

Nikki amefunguka hayo na kusema kuwa mchakato wa michujo inayotumika kupata wasomi imekuwa ikiwatenga wanafunzi wenyewe na hali hiyo inasababishwa na elimu inayotolewa ili kumkuza mwanafunzi.

Nikki amesema kwamba licha ya kulalamikiwa wanafunzi wanalega shule ni kutokana na kukosa mfumo bora wa kuwapelekea wao kutimiza ndoto zao zaidi ya kukaririshwa kuhusu elimu.

"Nikienda shuleni sasa hivi nikimuambia mwalimu anipe wanafunzi 10 wenye akili ataniletea anayejua hesabu, physics na masomo mengine lakini sitaletewa mwanafunzi anayejua kuchonga au anayejua muziki 'so' ikifika hapo unakuta mwanafunzi mwenyewe anaamua kufuata kile ambacho anaona anakiweza. Hivyo kwa mfumo huu hata wasanii wengi unakuta hawaendi shule" , amesema Nikki.

Aidha Nikki ameongeza, "Mtu kama Joh Makini na Rama Dee wana elimu za muziki ambayo wamejifunza, hivyo lazima watafanya vizuri, tofauti kama wangekuwa wanafanya kitu ambacho hawakipendi.