Alhamisi , 16th Feb , 2017

Msanii wa muziki Nay wa Mitego amesema kuwa ana mpango wa kumiliki kanisa siku za usoni kwa kuwa anaamini kwa sasa dini ndiyo biashara inayolipa zaidi ndani ya nchi na Afrika kwa ujumla.

Nay wa Mitego

Kauli hii imetoka kinywani mwa Nay wakati akijibu maswali ya mashabiki kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachoruka kila Jumatano kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV, baada ya kuchana mistari kadhaa iliyomo ndani ya ngoma yake mpya aliyoiachia leo mistari inayosema

Amesema kuwa kuwa yeye anatarajia kuwa mmiliki wa kanisa la imani anayoiamini yeye menyewe na kuongeza kuwa hiyo ni biashara inayolipa zaidi kwa sasa.

"Broo wewe kama una kiwanja chako jenga kanisa ni biashara inayolipa sana. Mimi natarajia siku za karibuni nitakuwa mmiliki wa kanisa kwa dini ninayoiamini mimi. Sitakuwa mchungaji lakini nitakuwa mmiliki wa kanisa" Nay aliwaeleza watazamaji wa KIKAANGONI.

Nay 'The true boy' ameongeza kwamba  katika orodha ya matajiri kwa sasa barani Afrika ni viongozi na wamiliki wa makanisa.