Alhamisi , 17th Jun , 2021

Muigizaji wa tamthilia ya vichekesho ya Mizengwe Mzee Sumaku amefunguka kusema Marehemu Mzee Matata alifahamu kifo chake kwani kabla ya umauti alimkabidhi mke na watoto wake wanne.

Kutoka kulia ni Safina, kati ni Mzee Matata kulia ni Mkwere

Mzee Sumaku anasema kauli hiyo aliambiwa Hospitali akiwa na Mke wa Mzee Matata na ilimuuma sana kwani alishajua anaashiria nini na alikuwa anaona hawezi kupona. 

"Matata na mimi ni zaidi ya ndugu, mara ya mwisho tulikuwa Temeke Hospitali alipozidiwa aliinita mbele ya Mkewe, akaniambia nikifa familia yangu nakuachia wewe naomba unilelee wanangu kile kitu kiliniuma sana, nilijaribu kumpa nguvu ila nilishajua anaashiria nini tayari alioona haponi" amesema Mzee Sumaku 

Mzee Matata alikuwa ana jumla ya watoto wanne na mke mmoja pia hana muda mrefu kwenye maisha yake ya ndoa.

Mazishi yaMzee Matata yanafanyika leo saa 7:00 Mchana kwenye Makaburi ya Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam.