Jumanne , 9th Mar , 2021

Mzee Kasauji maarufu kama Baba wa Kambo ambaye amefahamika zaidi kwenye mitandao ya kijamii amesema hawezi kuacha kutumia mitandao pia amepanga kufanya 'birthday party' kwenye mtandao wa TikTok.

Huyu Mzee Kisauji anayetrend

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Mzee Kisauji amesema atagharamia kila kitu kwenye kumbukumbu ya kuzaliwa kwake ambayo atakuwa anatimiza miaka 57 ili aifanyie TikTok kwa kuwa ndiyo umempa umaarufu.

"Nimezaliwa mwaka 1964, nina mke mmoja na watoto 7 birthday yangu nitaifanya TikTok nitaigaharamia kwa fedha zangu maana ninazo, wapenzi wangu nawaandalia kila kitu kwenye party yangu wao wasije na chochote na huko mitandaoni siwezi kutoka hata wanifanye nini" amesema Mzee Kisauji 

Mengine aliyoyazungumza tazama hapa chini kwenye video.