Baraka aikimbia suluhu na Rockstar

Sunday , 12th Nov , 2017

Meneja wa wasanii wa muziki wa bongo fleva ambaye pia ni mpiga picha maarufu bongo, Mx Carter, amesema alishawahi kuomba uongozi wa Rockstar 4000 uliokuwa unamsimamia Baraka kukaa chini kuzungumza ili kumaliza mgogoro wao, lakini aligomea jambo

Mx Carter ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye #eNewz ya East Africa Television, na kusema kwamba kwa sasa msanii huyo ana stress za muziki, hivyo aliona ni vyema kaa chini na uongozi wake wa zamani ili kumaliza tofauti zao zilizopo na kila mmoja aendelee na mambo yake kwa amani, lakini Baraka alikimbia jambo hilo bila sababu za msingi.

“Nilijaribu ku-'arange meeting' yeye na Rockstar wakae pamoja wamalize hili tatizo ili Baraka aendelee na situation zake na Rock Star waendelee na situation zao, Rockstar waliwekeza kwa Baraka walikuwa wanataka kurudisha fedha zao, lakini hiko kitu hakikutokea kiubishi ubishi tu”, amesema Mx Carter.

Hivi karibuni kumeibuka mgogoro mkubwa kati ya msanii huyo na lebo yake ya zamani RockStar 4000 na Mx Carter, akiwatuhumu kuingia kwenye acount yake ya YouTube na kupunguza views zake kwenye kazi yake mpya.