Alhamisi , 22nd Oct , 2020

Msanii Ice Boy amesema hamuigi, haigizi wala hajifananishi na marehemu Tupac Shakur ambaye alikuwa ni msanii wa HipHop nchini Marekani na alifahamika duniani kwa ujumla kutokana na nyimbo zake.

kushoto ni msanii Jux, kulia ni Ice Boy

Ice Boy ambaye anajulikana zaidi kwa majina ya Ice Pac au Tupac wa Iringa amesema yeye sio kama Jux ambaye huwa anampost Tupac mara kwa mara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ili kujifananisha naye.

"Mimi ndiyo msanii ninayevaa zaidi Africa, hapa Bongo nipo kwa makusudi kwa sababu nipo tofauti na wote kabisa maana ningezaliwa Ulaya ningefanana na watu wengi, mimi sijifananishi na Tupac ila nafanana naye na sijawahi kumpost kwenye page yangu, siigizi wala sijifananishi naye kwa chochote ila nafanana naye" amesema Ice Boy 

Zaidi mtazame hapa chini kwenye video.