Jumamosi , 22nd Apr , 2017

Msanii wa muziki miondoko ya mduara nchini, AT amchana vikali 'dancer' na msanii Msami kwa kumwambia kwake siyo mahali pakuchezea kama anavyodhania huku akimtaka aende kwa Alikiba kwakuwa ni mnyonge hata akitukanwa hukaa kimya.

Hayo yameibuka baada ya Msami kumtaka AT aboreshe kazi zake badala ya kulalamika kuwa kuna watu wanaobebwa huku akijitapa kuwa dancers wana maisha mazuri na mafanikio makubwa kumzidi yeye.

“Hawa watoto huku kwangu siyo pakuchezea, mchezeeni Alikiba mnyonge anakaa kimya hata mkimtukana hajibu kitu ila huku kwangu waachane napo siyo kwa kawaida na kama hawataki basi wajaribu zali kama wenzao halafu watapata majibu yao”. Alisema AT

Aidha AT alifika mbali zaidi kwa kusema yeye ni msanii bora kuliko anavyomchukulia kwa kuwa anaweza kucheza na ‘vocal sound’ kwa kuiga sauti  wasanii wakubwa huku akitolea mfano kwa Bi. Kidude, Oliver Mtukuzi pamoja na Chriss Brown

 “Wewe hunijui,  umeenda tu kuruka ruka sehemu umechukuliwa baadae umejiona umeimba chooni ukadhani unajua kuimba. Mimi mwenzio nimeenda chuoni”. Alisisitiza AT

Mbali na hilo AT aliwataka watu ambao wanatafuta majina kupitia yeye wakome kabisa tabia hiyo kwani yeye ni mtu mbaya akisema siku aachie mabomu yake hawataweza kuvumilia kwani watatafutana, hivyo kama wanataka kiki waende kwa Harmorapa lakini si kwake.