Jumanne , 26th Sep , 2017

Msanii Madee ambaye leo ameachia kazi yake mpya wa 'Sema' aliomshirikisha msanii wa kike Nandy, amesema anapata wakati mgumu sana kutoka kwa mama yake kwa kitendo chake cha kuwasaidia watu baki kuliko ndugu zake.

Madee ameyasema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba mama yake huwa anamshangaa sana kwa kitendo hicho, ambacho kimeweza kuibua vipaji vya wasanii hapa bongo, huku ndugu zake wa damu wakibaki bila msaada wowote, na kutoa sababu ya kuwasaidia watu hao.

"Unajua mimi mpaka mama yangu huwa ananilaumu kwa nini nasaidia watu baki alafu ndgugu zangu nawaacha, unajua muda mwengine kwa kuwasaidia hao watu mimi ndio napata riziki, na pia unakuta hao ndugu zangu sio wasanii, pengine msaada wanaohitaji ni pesa tu, sasa kama ni pesa mtu utampa kila siku lakini haimsaidii, kuliko yule anayetaka umsaidie kwa kumtengenezea njia za kuweza kupata hela mwenyewe", amesema Madee

Madee ameshasaidia baadhi ya vijana wengi na baadhi yao kufanikiwa, huku wengine bado wakiwa wanaendelea kupigana kutoka kwenye sanaa ya muziki, akiwemo Dogo Janja, Ray Vanny na Lulu Diva